Patrice Evra amewaasa wachezaji wenzake wa Manchester United, kuwa makini na kuendelea kukaza buti baada ya kuanza msimu mpya wa ligi kwa rekodi nzuri.
"Tunafanya na inaonekana kama rahisi, lakini si kweli." Alisema alipokuwa anaongea na gazeti la The Independent, "Ninawaheshimu sana Manchester City - wana kikosi makini sana."
"Walipoifunga Tottenham 5-1, tuliiangalia mechi na tukasema ni vyema tukacheza vizuri tukikutana na Arsenal - na tukafanikiwa kushinda kwa goli nane."
"Inaonekana kama ni mashindano kati ya timu hizi mbili, ila msisahaua Chelsea na Liverpool. Japokuwa, kila niwaonapo watu kitu cha kwanza kwao kuuliza ni tarehe ya mechi na wapinzani wetu."
No comments:
Post a Comment