Wednesday, September 7, 2011

Ferguson: Sneijder si wakufananishwa na Scholes

Xavi & Paul Scholes

KOCHA wa Klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson, amesema Wesley Sneijder asingeweza kuwa mtu sahihi kama mtu mbadala wa kumrithi Paul Scholes ndani ya Manchester United, huku akisisitiza ni wachezaji wa Barcelona pekee yaani Xavi na Andres Iniesta ndio umbao ungeweza kuwafananisha na mchezaji huyo na kiungo wa zamani wa Uingereza.
"Sneijder si aina ya mchezaji anayeweza kuwa mbadala wa Scholes," Ferguson alisema.

"Ni mchezaji mzuri, lakini hakuwa aina ya mchezaji tuliyekuwa tunamtafuta kuweza kumrith Scholes. Ni Xavi na Iniesta pekee ndio unaoweza kuwalinganisha na Scholes."

Hispania 6-0 Liechtenstein

Alvaro Negredo

Timu Taifa ya Hispania imeweza kupata ushindi wa 6-0 dhidi ya Liechtenstein.

David Villa aliingia wavuni mara mbili, Negredo naye akapiga bao mbili, huku Xavi na Sergio Ramos wakifunga goli moja moja.

Kwa ushindi huo Kikosi hicho cha Vicente Del Bosque, kimeweza fanikiwa kukata tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la mataifa ya Ulaya, waikiwa wamejikusanyia pointi 18 kutokana na mechi 6 walizocheza, wakifatiwa na Czech Republic kwenye nafasi ya pili.

33′ Negredo
37′ Negredo
44′ Xavi
52′ Sergio Ramos
60′ David Villa
79′ David Villa

Ronaldinho Arudi na Kuanza kwa Ushindi

Ronaldinho kwenye mechi Brazil na Ghana

Kwenye mechi yake ya kwanza baada ya miezi  zaidi ya 10, Ronaldinho amerudi tena akiwa timu ya taifa ya Brazil, akianza mwanzo mwisho kuisaidia nchi yake kuishinda 1-0 dhidi ya Ghana.

Mabadiliko ya Ratiba VPL


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya mabadiliko madogo ya ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kutokana na Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid ulioko mkoani Arusha kuwa na shughuli nyingine za kijamii.
 
Kati ya Septemba 7 na 8 mwaka huu, na Septemba 17 na 18 mwaka huu, uwanja huo utatumika kwa shughuli za dini na mashindano ya riadha ya Safari International Marathon.

Mabadiliko ya ratiba yanahusisha mechi zifuatazo na tarehe mpya zikiwa katika mabano; Septemba 7 mwaka huu mechi namba 20- Oljoro JKT vs Azam (Septemba 9), Septemba 10 mwaka huu mechi namba 22- Azam vs Simba (Septemba 11), Septemba 11 mwaka huu mechi namba 26- Ruvu Shooting vs Yanga (Septemba 10).
 
Septemba 17 mwaka huu mechi namba 38- Oljoro JKT vs African Lyon (Septemba 19), Septemba 21 mwaka huu mechi namba 43- Kagera Sugar vs Oljoro JKT (Septemba 22), Septemba 21 mwaka huu mechi namba 49- Ruvu Shooting vs African Lyon (Septemba 20) na Septemba 24 mwaka huu mechi namba 54- Toto Africans vs Oljoro JKT (Septemba 25).

Mchezaji Bora wa Wiki Goal.com

Cesc Fabregas

Cesc Fabregas, wiki hii amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mtandao maarufu wa Goal

Jina: Francesc "Cesc" Fàbregas i Soler
Klabu: Barcelona
Nchi:Hispania
Miaka: 24
Nafasi: Kiungo

Mafanikio: Amesaidia ushindi kwa Barcelona na timu ya Taifa ya Hispania

Del Piero: Sijaamua hatma yangu

 Alessandro Del Piero

Mchezaji mkongwe wa Juventus Alessandro Del Piero, amesema bado hajaamua kama ataendelea kucheza mpira baada ya msimu huu wa 2011-12.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36, bado yupo kwenye mkataba unaomuweka mpaka mwezi June mwakani pale Turin, ila inaelezwa kwamba mwisho wa mkataba huo haimaanishi kwamba na yeye atastaafu baada ya msimu huu.

"Kufikiria juu ya mwisho wangu kwenye soka , si kitu ambacho kinanichukulia muda kuamua. Bado sijaamua kama huu utakuwa ni mwisho wangu kucheza na Juventus," Del Piero alieleza La Gazzetta dello Sport.

"Kufikiria juu ya kwamba huu ni mwaka wangu wa mwisho inanifanya nijitoe kwa zaidi ya asilimia 200, nahitaji kumaliza kipindi changu nikiwa kwenye mafanikio ya juu."

Nikijaribu kuangalia nyuma miaka 20 iliyopita, nitaangalia nikiwa nimeridhika sana."

Del Piero alianza kucheza kwenye kiwango cha juu akiwa KlabuPadova, ila akajiunga na Juventus mnamo 1993. Mchezaji huyo mpaka sasa ameweza kucheza jumla ya mechi 600 kwa timu hiyo ya Serie A na kuifungia jumla ya magoli 285.

Capello: Barcelona Watafungika

Fabio Capello

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello amesema kwamba, anaamini haitachukua muda kwa timu kupata jibu juu ya aina ya mpira ambao timu ya Barcelona inaucheza.

Timu hiyo ya Catalans inaaminika na watu wengi kwamba ni timu kali ambayo haijawahi  tokea duniani, ila Capello anaamini kwamba utawala wao hautakuwa wa milele.

"Naweza kumuona mtu anayeweza kuizuia Barcelona kwa siku za mbele? Nafikiri ndio itawezekana, sababu tuna bahati kwamba tunaweza kuwasoma wapinzani," Capello alinikuliwa kwenye mtandao wa FIFA.

"Utapata ufumbuzi wa namna ya kuizuia Barcelona, kwa kuelewa uwezo wao. Utajifunza mengi, ukiangalia mchezo wao kwenye mikanda. Naamini baadhi ya timu zitapata dawa ya kuifunga."

Pia anaamini kwamba taratibu kama ilivyo asili ya mchezo, kiwango chao kinaweza kushuka.

Akaendelea kusema "Unapokuwa unashinda mara nyingi, wakati mwengine unakosa kitu kinachokufanya uwe makini kwa kila mchezo kuweza kushinda, wachezaji wengine pia wanazeeka kimchezo."

Barcelona wameshinda Kombe la mabingwa msimu uliopita, na wameanza msimu mpya wa2011-12, wakiwafunga wapinzani wao Real Madrid kwenye Supercop ya nchini kwao Hispania, wakaja kuwafunga Porto kwenye Supercup ya Ulaya.

Santos: Hakuna makubaliano ya Neymer kuuzwa

Neymer

Klabu ya Santos  ya nchini Brazil imesema haijafikia makubaliano na timu yoyote kumuuza mshambuliaji wake Neymar.

Klabu hiyo imetoa tamko hilo Jana Jumapili kwenye taarifa ndefu waliyoitoa kwenye Mtandao wake, taarifa hiyo imesisitiza kwamba hakuna dili yoyote ambayo wamefikia na Barcelona juu ya kumuhamisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19, ili aweze kuhamia Camp Nou ifikapo mwaka 2013.

"Kutokana na sababu binafsi zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya habari hivi karibuni kuhusiana na Neymar, Santos Futebol Clube inapenda kutoa tamko rasmi kwamba, maelezo yanayotolewa na vyombo hivyo juu ya mustakabali wa Neymer sio za kweli” taarifa hiyo ilisema.

"Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu mara zote imekuwa na nia njema ya kuendelea kubaki na Neymer kwenye timu.”

Taarifa hiyo imekuja baada ya gazeti la Estadao siku ya Jumamosi kuandika kwamba, Santos na Barcelona wamefikia makubaliano ya awali kwa Neymar kujiunga na mabingwa Hispania na Ulaya baada ya miaka miwili toka sasa.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Bazil amekuwa akihusishwa na kuhamia Barcelona na kwa mahasimu wao Real Madrid katika kipindi cha majira ya joto, huku baadhi ya timu nyingine za Bara la Ulaya nazo zikihusishwa juu ya mpango huo.

Mara zote Neymer amekuwa akisisitiza kwamba kwa muda huu angependa kuendelea kucheza nchini mwake Brazil.

Terry: Don't write off Lampard

Terry & Lampard

England captain John Terry has voiced his full support for dropped midfielder Frank Lampard.

An injury-free Lampard was left out of a competitive England starting XI for the first time since 2007 with a midfield trio of Scott Parker, Gareth Barryand Ashley Young preferred for the 3-0 Euro 2012 qualifier win over Bulgaria last Friday.

There have been suggestions that Lampard's exclusion could be the beginning of the end of the 33-year-old's international career, but his Chelsea team-mate Terry has issued a warning to the doubters.

Twiga Stars yalala dhidi ya Ghana

 Wachezaji wa Twiga Stars

Timu ya wanawake ya Taifa ya Tanzania (Twiga Stars) imepoteza mechi yake ya kwanza ya michezo ya All Africa Games (AAG) baada ya kufungwa mabao 2-1 na Ghana katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Machava, jijini Maputo.

Kwa mujibu wa Meneja wa Twiga Stars, Furaha Francis hadi mapumziko timu hiyo ilikuwa nyuma kwa bao 1-0. Mwanahamisi Shuruwa aliisawazishia Twiga Stars dakika ya 85, lakini Ghana ikapata bao la pili dakika tatu kabla ya filimbi ya mwisho.

Twiga Stars itacheza mechi yake ya pili Septemba 8 mwaka huu dhidi Afrika Kusini. 

TFF yatangaza mapato ya pambano la Stars


Pambano la mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Algeria (Desert Warriors) limeingiza sh.148,220,000.

Mechi hiyo ilichezwa Septemba 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mashabiki waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo ni 29,892.

Meireles akana Pesa kumuondoa Liverpool

Raul Meireles

Mchezaji wa kimataifa wa Ureno Raul Meireles, amesisitiza kwamba hela si kitu ambacho kilimshawishi kufanya uhamisho wa kushtukiza toka Liverpool na kuhamia Chelsea.

"Haya ni mambo yanayotokea kwenye mpira wa miguu. Nitasema vitu vizuri tu kuhusu Liverpool, nilikuwa na mwaka mmoja mzuri," Meireles aliieleza *RTPN*.

"Watu wanafikiri mimi ni Yuda na nilihama kwa sababu ya hela. Hiyo haikuwa sababu, nitaelezea wakati mwengine, kwa sasa bado ni mapema.

Sneijder: Mourinho aliniambia nibaki Inter

Wesley Sneijder

Nyota wa Klabu ya Inter Milan Wesley Sneijder, amefunguka tena na safari hii akisema Kocha wake wa zamani Jose Mourinho, alimwambia awatose Manchester United na aendelee kubaki San Siro.

"Mourinho alinipigia simu akaniambia hivyo. Jamaa ana moyo na timu ya Inter na mara zote amekuwa akinieleza nibaki," Sneijder alilieleza *La Gazzetta dello Sport*.

"Niko na furaha kwa kubaki hapa, sikuwahi kutaka kuondoka na sitaki kuendelea kuzungumzia kuhusu Manchester United."

Barcelona: Fabregas Ana Thamani ya £53m

Cesc Fabregas  

Makamu wa Rais wa Klabu ya Barcelona Josep Maria Bartomeu, anaamini kwamba Cesc Fabregas ana thamani ya £53ml, hela ambayo klabu yake ya awali Arsenal ilikuwa inahitaji kuweza kumuuza mchezaji huyo kwa Barca.

Makamu wa Rais huyo amesema, katika kipindi kifupi alichomuona akiitumikia Barcelona na Hispania kwa ujumla, amemkubali sana.

"Baada ya kuona kazi anayoifanya toka awasili hapa, hakika Cesc thamani yake inafika €60ml sawa na £53ml ambazo Arsenal walizihitaji," alisema Bartomeu.


Wilshere Nje ya Uwanja Mpaka November

Jack Wilshere

Mchezaji Chipukizi Nyota wa Arsenal Jack Wilshere, ataendelea kuwa nje ya dimba kwa miezi miwili zaidi, hii ni kutokana na kutonesha enka yake ya mguu wa kulia.

Wilshere amekuwa nje ya uwanja kwa kipindi sasa, na hakuwahi kuhusishwa na mechi yoyote ngumu ambayo timu yake ilishiriki toka msimu mpya uanze, na hii ni kutokana na timu hiyo kutotaka kumuwahisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19.

Kolo Toure Ndani, Hargreaves Nje Kikosi Cha Man City

Kolo Toure

Klabu ya Manchester City, imetaja kikosi cha wachezaji 23 watakaoshiriki kwenye mashindano ya Kombe la Mabingwa Barani Ulaya, huku kiungo aliyesajiliwa hivi karibuni Owen Hargreaves akienguliwa kwenye kikosi hicho.

Kiungo huyo ameshindwa kujumuishwa kwenye kwenye kikosi cha wachezaji 23 wa Roberto Mancini licha ya hivi karibuni kusajiliwa na timu hiyo.

Beki Kolo Toure amejumuishwa kwenye kikosi baada ya kuwa nje ya Uwanja kwa Miezi sita kutokana na kesi iliyokuwa inamkabili ya kutumia madawa.

Mchezaji mwingine wa timu hiyo Wayne Bridge, ametoswa kwenye kikosi hicho.

Gerrard kurudi dimbani Sept. 18

Steven Gerrard
 
MCHEZAJI wa timu ya Liverpool Steven Gerrard, yuko karibu kurudi uwanjani baada ya kuwa nje ya dimba kwa kipindi cha miezi mitano kutokana na majeraha yaliyokuwa yanamkabili.
 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, ameshindwa kuichezea timu Liverpool na timu ya Taifa ya Uingereza toka mwezi wa March kutokana na upasuaji uliofanywa kwenye goti lake.