Fabio Capello
Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello amesema kwamba, anaamini haitachukua muda kwa timu kupata jibu juu ya aina ya mpira ambao timu ya Barcelona inaucheza.
Timu hiyo ya Catalans inaaminika na watu wengi kwamba ni timu kali ambayo haijawahi tokea duniani, ila Capello anaamini kwamba utawala wao hautakuwa wa milele.
"Naweza kumuona mtu anayeweza kuizuia Barcelona kwa siku za mbele? Nafikiri ndio itawezekana, sababu tuna bahati kwamba tunaweza kuwasoma wapinzani," Capello alinikuliwa kwenye mtandao wa FIFA.
"Utapata ufumbuzi wa namna ya kuizuia Barcelona, kwa kuelewa uwezo wao. Utajifunza mengi, ukiangalia mchezo wao kwenye mikanda. Naamini baadhi ya timu zitapata dawa ya kuifunga."
Pia anaamini kwamba taratibu kama ilivyo asili ya mchezo, kiwango chao kinaweza kushuka.
Akaendelea kusema "Unapokuwa unashinda mara nyingi, wakati mwengine unakosa kitu kinachokufanya uwe makini kwa kila mchezo kuweza kushinda, wachezaji wengine pia wanazeeka kimchezo."
Barcelona wameshinda Kombe la mabingwa msimu uliopita, na wameanza msimu mpya wa2011-12, wakiwafunga wapinzani wao Real Madrid kwenye Supercop ya nchini kwao Hispania, wakaja kuwafunga Porto kwenye Supercup ya Ulaya.
No comments:
Post a Comment