Klabu ya Barcelona imetangaza kwenye mtandao wake kwamba, Andres Iniesta atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja.
Kiungo huyo aliumia dakika 5 kabla ya mapumziko, kwenye mechi ambayo timu yake ilitoka sare ya 2-2 na AC Milan, katika michuano ya Kombe la mabingwa Barani Ulaya siku ya Jumanne.
Iniesta atakosa mechi dhidi ya Osasuna, Valencia, Atletico Madrid, BATE Borisov na Sporting Gijon.
Mchezaji huyo anategemea kurudi tena uwanjani kwenye mechi ya michuano ya Euro 2012, ambapo timu ya Hispania itakapocheza na Czech Republic na Scotland, mnamo tarehe 7 na 11 Oktoba.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ameweza kucheza jumla ya mechi 6 kwa klabu msimu huu, huku akikamilisha wastani wa dakika 469 uwanjani.