Wednesday, September 7, 2011

Kolo Toure Ndani, Hargreaves Nje Kikosi Cha Man City

Kolo Toure

Klabu ya Manchester City, imetaja kikosi cha wachezaji 23 watakaoshiriki kwenye mashindano ya Kombe la Mabingwa Barani Ulaya, huku kiungo aliyesajiliwa hivi karibuni Owen Hargreaves akienguliwa kwenye kikosi hicho.

Kiungo huyo ameshindwa kujumuishwa kwenye kwenye kikosi cha wachezaji 23 wa Roberto Mancini licha ya hivi karibuni kusajiliwa na timu hiyo.

Beki Kolo Toure amejumuishwa kwenye kikosi baada ya kuwa nje ya Uwanja kwa Miezi sita kutokana na kesi iliyokuwa inamkabili ya kutumia madawa.

Mchezaji mwingine wa timu hiyo Wayne Bridge, ametoswa kwenye kikosi hicho.

No comments:

Post a Comment