Andre Ayew
Mchezaji nyota wa Timu ya Taifa ya Ghana Andre Ayew, atakosa mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, wakati timu yake ya Marseille itakapokuwa inacheza na Olympiakos siku ya Jumanne.
Ayew 21, anasumbuliwa na maumivu ya kifundo, yatamsababisha pia asiwepo kwenye mechi ya kwanza ya Ligue 1, ambayo Timu yake itacheza dhidi ya Stade Rennes wekiendi hii.
"Andre Ayew anategemea kuwa nje ya uwanja kwa siku 10, baada ya kuumia kwenye mechi aliyokuwa anaitumikia Ghana," FA ya Ghana imeeleza kwenye mtandao wake leo.
"Mchezaji huyo wa Marseille alipata jeraha hilo wakati Ghana ilipokuwa inacheza na Swaziland, kwenye mechi ya kusaka nafasi ya kushiriki Kombe la Mataifa ya Afrika Ijumaa iliyopita." Taarifa hiyo ilisema.
No comments:
Post a Comment