Mohamed Bin Hammam
Shauri la aliyekuwa mgombea nafasi ya Urais wa FIFA Mohamed Bin Hammam, juu ya kupinga adhabu ya kifungo cha maisha aliyopewa kutojihusisha na masuala ya mpira, limepangwa kusikilizwa wiki ijayo.
FIFA wamethibitisha.
Kamati ya rufaa ya FIFA, inategemea kusikiliza shauri hilo siku ya Alhamisi, September 15, ambapo Bin Hammam anapinga adhabu hiyo, iliyotolewa na kamati ya maadili ya Shirikisho hilo mnamo mwezi July.
Shauri hilo linaweza kamilika siku hiyo japo kuna uwezekano linaweza kwenda mpaka September 16.
No comments:
Post a Comment