Rooney & Hernandez
Wayne Rooney amesema, angependa kuungana na mchezaji mwenzake Javier Hernandez kwenye safu ya ushambulizi ya timu hiyo mapema zaidi.
Wachezaji hao wawili, msimu uliopita wa EPL walitengeneza safu kali ya ushambuliaji, safu iliyosaidia kuipa Manchester United ubingwa wake wa 19 wa Ligi hiyo.
"Naamini tulichokifanya na Hernandez msimu uliopita tutakifanya pia msimu huu, tutafunga magoli mengi," Rooney aliieleza MUTV.
"Hakika watu wanamfahamu kwa sasa ila, kama ukiangalia wachezaji wakali Duniani, huwa wanafahamu wanacheza na nani na ni ngumu kuwazuia.
"Mienendo yake ndani ya uwanja ni mizuri, na ni ngumu kuizuia. Si rahisi kwa wachezaji kumzuia, wawe wanamfahamua ama kinyume chake.
"Ni vizuri kuwa na mwenza ambaye amefika kwenye timu, ambaye anaweza kuongea Kingereza kizuri na kila wakati ana tabasamu." Alisema Rooney.
No comments:
Post a Comment