Mario Balotelli
Mikasa inayomkumba Mario Balotelli toka ajiunge na Klabu ya Manchester City imechukua hatua nyingine, safari hii mchezaji anatakiwa na Jeshi la Polisi la nchini Italia kuelezea mahusiano yake na Kundi la Kijasusi la Mafia.
Balotelli, ambaye amejiunga na Klabu hiyo kwa wa £24 ml toka Inter Milan mnamo mwaka jana, ameitwa kama shahidi na waendesha mashtaka wa jiji la Naples, lengo likiwa ni kuweza kusaidia uchunguzi unaoikabili kundi la Mafia.
Inasemekana mchezaji huyo, alionekana akiwa sambamba kwenye msafara wa moja kati ya makundi ya kiharifu yaliyopo jijini Naples, makundi yanayoongozwa na Mario Iorio, mmoja kati ya watu wanaojishughulisha na biashara ya kusambaza vyakula.
Huku ikielezwa, Lorio anahusishwa na kashfa ya utengenezaji noti bandia, kesi yake ikiwa inaendelea.
"Hakuna kitu cha kuogopa, niko poa, sikuwa na wazo na watu waliokuwa wanapita karibu yangu ni kina nani," Balotelli alisema alipoulizwa kuhusiana na ishu hiyo.
"Siku ile kulikuwa na watu wengi karibu yangu, najisikia vibaya sababu inaweza kuithiri familia yangu, nilichokuwa nataka nione pale ni namna gani lile eneo linafanana na vile ambavyo huwa naliona kwenye filamu ya Gomorrah."
No comments:
Post a Comment