Pep Guardiola
Kocha wa Klabu ya Barcelona Pep Guardiola, amepewa Tunzo ya Dhahabu ya mafanikio na Bunge la Catalonia.
Tunzo hiyo inatambua mchango wake toka alipoichukua timu hiyo kipindi cha majira ya joto ya mwaka 2008, baada ya kuwa kocha wa timu B ya Barcelona kwa mwaka mmoja.
"Nilichaguliwa kuwa Kocha wa Barca na faida ilikuwa ni kwa wale walionichagua, huku hii ikiwa njia nzuri ya kukabiliana na kazi yangu," alisema.
Guardiola ameiongoza na kuipa Barca jumla ya makombe 12, mawili ya Kombe la Mabingwa Ulaya, na matatu yakiwa ni mataji ya La Liga.
No comments:
Post a Comment