Fernando Torres
Fernando Torres ameelezwa na Kocha wa Timu ya Taifa lake Vicente del Bosque kwamba, anaweza kupoteza nafasi yake kwenye kikosi hicho, kama atashindwa kufunga magoli mara kwa mara kwenye timu yake ya Chelsea .
Nafasi yake kwenye timu ya Chelsea inatishiwa na uwepo wa wachezaji kama Didier Drogba, Nicolas Anelka na Romelu Lukaku, kitu ambacho kinatisha nafasi yake pia kwenye timu ya taifa. lake.
Del Bosque hakumpa nafasi Torres hata yakuwepo kwenye benchi, kwenye mechi ambayo Hispania ilishinda kwa magoli 6-0 dhidi ya Liechtenstein, kitendo kilichomfanya mshambuliaji huyo kuangalia mechi hiyo akiwa jukwaaini.
"Torres ni mchezaji muhimu, ila wale wanaofanya vizuri kwenye klabu zao ndio wataoitwa timu ya Taifa, na si kinyume na hapo," alisema Del Bosque.
Torres hajaifungia timu yake ya taifa toka alipofunga kwenye mechi dhidi ya Liechtenstein miezi 12 iliyopita.
No comments:
Post a Comment