Roberto Mancini
Meneja wa Timu ya Manchester City Roberto Mancini, amesema mwanzoni nia yake kuu ilikuwa ni kumsajili mchezaji wa Roma Daniele de Rossi au mchezaji wa Real Madrid Fernando Gago - ila akasema sababu za kifedha ndizo zilizosababisha amsajili Owen Hargreaves.
Mancini aliieleza the Independent: "Gago ndiye mchezaji tuliyemtaka kwa udi na uvumba, hatukutaka tutumie hela zaidi ya ile tuliyoipanga.
"De Rossi ni mmoja kati ya viungo wazuri hapa Duniani, ila siamini kama anaweza kuondoka Roma. Kwa hiyo kwenye kiungo tukaamua kumsajili Hargreaves, ambaye yuko nje ya mkataba.''
No comments:
Post a Comment