Andre Villas-Boas
Kocha wa Timu ya Chelsea Mreno Andre Villas-Boas, amesema baada ya kumsajili aliyekuwa kiungo wa timu ya Liverpool Raul Meireles, hatomuhitaji tena mchezaji aliyekuwa anamtaka kwa kipindi kirefu, kiungo mchezeshaji wa timu ya Tottenham Hotspur Luka Modric.
Alipoulizwa kama Chelsea watarudi na kumsajili tena mchezaji huyo wa Tottenham katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo mwezi January, Villas-Boas alisema: "Hapana, sidhani. Soko limeshafungwa na siwezi bashiri kitakachotokea mwezi January."
Vile vile kocha huyo, Villas-Boas amesikitishwa kwa kushindwa kumsajili beki wa kushoto toka Uruguay Alvaro Pereira, ambaye anakipiga na Klabu ya Porto.
"Tulikuwa mbali kuweza kufikia kiwango cha matakwa ya Porto kwa mchezaji huyo. Niko na furaha nikiwa na Ashley Cole na Ryan Bertrand."
Wakati huo huo, Didier Drogba, anakimbizana na muda kuweza kuwa fiti ili aweze kuwemo kwenye mechi ambayo Chelsea watacheza na Manchester United.
Kocha wa Blues Andre Villas-Boas amesema, mshambuliaji huyo atakosa mechi ya Jumamosi hii dhidi ya Sunderland, na ile ya Jumanne ya Kombe la Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya Bayer Leverkusen.
No comments:
Post a Comment