Per Mertesacker
Beki mpya wa Arsenal Mjerumani Per Mertesacker, anaamini ataweza kufata nyayo za beki wazamani wa timu hiyo Tony Adams, hii ni katika kuelekea kwenye mechi yake ya kwanza akiwa na washika bunduki wa Emirate siku ya Jumamosi dhidi ya Swansea.
Mertesacker anatakiwa aendane na mfumo wa vijana wa Wenger haraka, beki wa timu hiyo Thomas Vermaelen yuko atakuwa nje ya dimba kwa wiki sita, baada a kufanyiwa upasuaji wa enka siku ya Jumatatu.
Mjerumani huyo, ambaye amejiunga na Klabu hiyo akitokea Werder Bremen kwa gharama ya £8 ml, anataka kuwa sehemu ya wachezaji watakao rudisha mafanikio ya timu ya Arsenal.
Tonny Adam alikuwa nahodha wa timu hiyo kwenye moja kati ya vipindi vya mafanikio ya Klabu hiyo, Mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal aliiwezesha timu hiyo kushinda vikombe Vinne vya Ligi, huku wakati flani akiweza kubeba kombe hilo mara mbili mfululizo chini ya Wenger.
"Hatukuwa na taswira yake kwenye Tv, ila Adam aliheshimika sana hapa, yeye ni mtu muhimu kwangu," Mertesacker aliueleza mtandao wa Klabu ya hiyo.
"Nilipokuwa naangalia Ligi ya Uingereza, mara nyingi nilikuwa nawaatazama Arsenal, hakika alikuwa ni beki mzuri sana, kipindi hicho nikiwa na miaka 10 au 12 hivi, nawapenda wachezaji kama Adams sana tu – Nimekuwa nikifurahi kuwangalia kwa miaka mingi.
" Natumai nitaongeza kiwango changu hapa na kuwa bora na bora – nataka niwe mtu muhimu kwenye timu."
No comments:
Post a Comment